Wananchi wa Kitongoji cha Kengereka Kata ya Muungano Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kitongoji hicho.
Wametoa shukrani hizo wakati wa ziara ya Mkuuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu ambayo imefanyika leo tarehe 15/08/2023 wakati alipokuwa akitembelea ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Kengereka iliyopo Katika kata ya Muungano.
Wananchi hao wamesema wanampongeza Rais kwa kuweka kipaumbele suala la elimu kwa kukarabati, kuongeza miundombinu na kujenga shule mpya sehemu zenye uhitaji.
Kwa upande wao wanafunzi wa shule hiyo wamesema ujenzi wa vyumba hivyo vinne vya madarasa na vyoo utapunguza changamoto ya msongomano darasani na kuwasihi wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni hapo.
Akiongea kwa niaba ya wenzao Eliana Joseph amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga na kuboresha sekta ya elimu.
Mradi huo wa uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu shule ya Msingi Kengereka unajumuisha ujenzi wa madarasa 4 na matundu 3 ya choo kwa gharama ya shilingi 106,300,000.00.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai