Wananchi na wakazi wa kijiji cha Mlima Shabaha Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwasogezea karibu huduma ya umeme.
Pongezi hizo zimetolewa mbele ya Kamati ya Siasa wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai katika mradi wa umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA awamu ya Pili katika eneo la Mlima Shabaha ukiwa umelenga kuwanufaisha wananchi wa Mlima Shabaha na eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda lililopo nyuma ya Mashine Tools.
Mmoja wa wanachi hao alisema, ‘’Kabla ya kukamilika kwa mradi huu tulikua tunashindwa kufanya baadhi ya shughuli za kimaendeleo hususani zinazoendeshwa kwa kutegemea mifumo ya umeme na kushindwa kuendana na kasi ya maendeleo ya Serikali’
‘’Huduma hii tulikua tukiisubiri kwa muda mrefu lakini leo hii tunaishukuru Serikali yetu kua sikivu kwakufanikisha hili”: alisema Laizer.
Kusogezwa karibu kwa mradi huu kutawawezesha wananchi hao kujiajiri na jambo litakalowasidia kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya shughuli tofautitofauti.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai