Wauguzi Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia maadili, taratibu na sheria za taaluma yao.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Klimanjaro Mhe. Nurdin Babu wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Kisiki kilichopo katika kata ya Machame Kaskazini wilayani Hai.
Babu amesema kuna baadhi ya wauguzi wanaotoa lugha chafu kwa wagonjwa hali inayosababisha wananchi kulalamikia kero hiyo kwa viongozi na kuongeza kuwa hatosita kuwachukulia hatua wauguzi hao wanaokiuka maadili ya kazi.
Hata hivyo wananchi wa kata hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha miundombinu ya hospitali hiyo kwa kuwajengea jengo la upasuaji ambapo hapo awali walikuwa wakifuata huduma hiyo katika hospitali nyingine.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai