JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MADAKTARI
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira ya Madaktari 610 watakaofanya kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini. Hivyo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuwatangazia Madaktari wa Binadamu na Meno waliohitimu katika vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali kuwasilisha maombi ya nafasi za ajira kuanzia leo tarehe 24/03/2020 ili kujaza nafasi mbalimbali katika Hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya kama ifuatavyo:-
1. Daktari Daraja la II /Daktari wa Meno Daraja la II (Nafasi 610) Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu/Meno kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi kwa vitendo (Internship) kwa muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
SIFA ZA MWOMBAJI; i. Awe raia wa Tanzania; ii. Awe na umri usiozidi miaka 45; iii. Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea; iv. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au asiwe Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali; v. Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini; na vi. Asiwe na check namba.
MAOMBI YOTE YAAMBATISHWE NA NYARAKA ZIFUATAZO: i. Barua ya maombi ya kazi ikieleza Mikoa mitatu ambayo mwombaji angependa kupangiwa kufanya kazi katika moja ya Halmashauri zake; ii. Nakala ya cheti cha kidato cha nne/sita; iii. Nakala za Vyeti vya Taaluma;
2
iv. Nakala ya cheti cha kuzaliwa; v. Nakala ya cheti cha usajili kamili (Full Registration) au Leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika; na vi. Maelezo binafsi (CV), yakionesha umri, anuani kamili na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/namba za simu za kiganjani za wadhamini wasiopungua wawili.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi Halmashauri yoyote watakayopangiwa; ii. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi na mashirika/taasisi zilizoingia ubia na Serikali; iii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wanatakiwa waambatishe Equivalent Certificate kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU); na iv. Waombaji watakaotuma/waliotuma maombi yao ya kazi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto hawapaswi kuomba nafasi hizi za kazi zilizotangazwa kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ifuatayo: ajira.tamisemi.go.tz.
Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisini hayatafanyiwa kazi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Aprili, 2020 saa 9:30 alasiri.
Tangazo hili linapatikana katika tovuti yetu www.tamisemi.go.tz
http://tamisemi.go.tz/announcement/tangazo-la-kazi-kada-ya-afya
MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE
http://ajira.tamisemi.go.tz/#!/auth
Limetolewa na: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mji wa Serikali – Mtumba, S.L.P 1923, 41185 DODOMA.
24 Machi, 2020
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai