T A N G A Z O
HUDUMA YA KUPIMA MACHO BURE HOSPITALI YA WILAYA YA HAI
Wananchi wote mnatangaziwa kuwa huduma ya matibabu ya macho itatolewa BURE siku ya Jumanne tarehe 16/10/2018 kuanzia Saa 3:00 asubuhi hadi Saa 9:30 alasiri katika Hospitali ya Wilaya ya Hai.
Huduma hii itatolewa na Madaktari wa Macho wa Wilaya wakishirikiana na madakatari wabobezi wa macho Mkoa.
Wananchi watakaogundulika kuwa na matatizo ya macho watatakiwa kuchangia gharama za dawa na miwani na watakaokuwa na mtoto wa jicho (Cataract) watapangiwa siku ya upasuaji Hospitali ya Rufaa Mkoa Mawenzi.
KAULI MBIU: “Afya ya Macho; Huduma ya Macho Popote Ulipo”
Afya Yangu, Mtaji Wangu.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na DR Mwanga kwa namba za simu 0753499659.
|
Tangazo hili limetolewa na
Riziki G. Lesuya
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya
HAI
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai