A. Mahitaji Muhimu wakati kupata Leseni mpya ya Biashara.
1. Fomu ya Maombi (Inapatikana Ofisi ya Biashara Wilaya)
2. Jina la/Majina ya Baishara (yataonekana kwenye leseni
yako).
3. Kama ni kampuni aje na nakala ya cheti ya usajili wa
BRELA (Certificate of Registration)
4. Nakala ya cheti cha namba ya utambulisho wa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA (TIN NUMBER).
5. Cheti Orijino cha kuonyesha hudaiwi kodi (Tax Clearance
Certificate) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
6. Ada ya Maombi Tsh.1, 000/-
7. Ada za leseni kwa Mwaka (zinatofautina kulingana na aina ya
baishara)
Kwa usajili wa bishara za zilizopo chini ya Mamlaka nyingine Mfano Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), biashara hizo ni kama vile Maduaka ya Dawa za Binadamu, Vinywaji laini, Maduka ya Pembejeo za Kilimo na Mifugo pamoja na maduka ya vyakula mnatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatavyo:-
(a). Cheti cha Cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) au
Mamlaka nyingine
(b) Cheti cha Vipimo vya Afya
(c) Pamoja na viambatanishi vingine vilivyotajwa hapo juu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa Biashara Wilaya ya Hai kwa simu namba:
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai