Ofisi ya waziri mkuu imetoa mafunzo kwa wataalamu wa sekta mbalimbali pamoja na asasi za kiraia Wilayani Hai yenye lengo la kutoa elimu ya namna sahihi ya kukabiliana na majanga yanayosababishwa na magonjwa yanayohusisha wanyama, mimea pamoja na binadamu.
Mafunzo hayo yanatolewa katika nchi 14 barani Afrika, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi hizo yakilenga Mikoa minne ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro yenye lengo la kutengeneza timu itakayojulikana kama Timu ya afya Moja yenye jukumu la kuratibu vikao na kusimamia shughuli za afya moja, kuandaa mipango mikakati na upatikanaji wa fedha kwajili ya utekelezaji wa shughuli za afya moja.
Dtk. Henry Kissinga anaetokea katika Ofisi ya waziri mkuu idara ya Menejimenti ya maafa akiwa ni miongoni mwa waalimu waliotoa mafunzo
hayo katika kikao hicho amesema,
"Tuko hapa kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu kutoka katika sekta ya afya ya binadamu, afya ya mifugo, mazingira, Kilimo na maliasili ili kukabiliana na magonjwa hususani magonjwa yanayotoka kwa wanyama kuja kwa binadamui (Zoonotic) ili waweze kutumia dhana ya afya moja itakayo zisaidia sekta hizo kukabiliana na magonjwa pamoja na kuzuia na kuhakikisha kua jamii inakua salama, vilevile wanyama pamoja na mazingira": Kissinga
Afisa maafa (w) Hai, Msafiri Msuya ameipongeza Ofisi ya waziri mkuu kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamewajengea uelewa wa dhana ya afya Moja katika kukabiliana na majanga mbalimbali.
Ameongezea kwa kusema, "Elimu hii itatusaidia kwasababu tulipokua tukifanya kazi Kila mmoja alikua anapita katika njia yake, Sasa tunakwenda kufanya kazi kama timu Moja jambo ambalo litasaidia
kutokutumia rasilimali nyingi katika jambo Moja kama ilivyokua hapo awali".
Vilevile, Helga Simon aliyekua mshiriki katika mafunzo hayo akitokea idara ya huduma ya afya ustawi wa jamii na lishe (w) Hai amesema, mafunzo hayo yamewakumbusha majukumu yaliyopo kwenye idara ya afya na katika idara "nyingine kufanya kazi kwa
kushirikiana ili kutoa huduma kwa ueledi hususani kwenye magonjwa ya mlipuko kwani watatoa huduma kwa kushirikiana na idara nyingine kwaajili ya kuleta matokeo Mazuri kwa huduma endelevu. Mfumo huu unasaidia pia kuhakikisha sisi wote tunalenga jambo Moja, pia kua na takwimu sahihi katika utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ya Wilaya": Helga.
Afya Moja ni dhana ya kimataifa iliyoridhiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Programu ya Kimataifa ya Mazingira (UNEP) kupitia “Global Health Security Agenda” (GHSA) na wadau wengine wa Afya duniani kote.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai