Serikali imetoa kiasi cha shilingi 251,269,712.27 kupitia mradi endelevu ya Maji na Usafi wa Vijijini (SRWSS) awamu ya pili katika Zahanati 5 wilayani Hai.
Miradi itakayotekelezwa ni pamoja Zahanati ya KIA shilingi 46,000,000.000, Zahanati Chemka 39, 000, 000, 00, Narumu 29,000,000.00, Kwatito 46,000,000.00 na Kwenshoo 22,000,000.00.
Akisoma taarifa hiyo katika kikao cha kamati ya Afya Msingi , Afisa Afya wilaya ya Hai Fabian Muibo amesema miradi hiyo itatekelezwa kutokana na uhitaji wa kituo ambapo miongoni mwa kazi zitakazofanyika ni ujenzi wa vyoo, mashimo ya maji taka,mnara wa tenki la maji ,kichomea taka pamoja na choo katika chumba cha kujifungulia.
Muibo amemshukuru mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo jambo ambalo litaendelea kuboresha kiwango.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa ametaka uwajibikaji katika usimamizi wa miradi hiyo ya wamu ya pili na kuhakikisha inamaliza kwa wakati uliokusidiwa na kwa ubora huku akiwapongeza Divisheni ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe wa kusimamia vema miradi ya awamau ya kwanza.
“tunawapongeza sana Mganga Mkuu, Mkurugenzi na watumishi wote wa afya kwani kuna mabadiliko sana katika utoaji wa huduma na changamoto ndogondogo ziendelee kufanyiwa kazi
pamoja na huduma tuendelee kupanda miti kwenye vituo vya afya na Zahanati ,tupopanda miti tupande na miti ya matunda,utunzaji wa mazingira uendee kwa kasi katika vituo vyote vya kutolea huduma
Katika utekelezaji mardi wa SRWSS awamu ya kwanza, halmashauri ya wilaya ya Hai ilipokea kiasi cha shilingi 160,723,614.00 ambazo zilielekezwa katika Zahanati 4 ambazo ni Bomangombe 53,313,000.000, Rundugai 42,143,114.00, Lambo 35,666,500.00 na Nkwenshoo 29,601,000.00.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai