Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amesema kuwa wilaya hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kusogeza maendeleo kwa wananchi ambapo tayari wamempata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya nyerere Bomang’ombe yenye urefu wa mita 700.
Rutaraka ambaye ni diwani wa kata ya Muungano, ameeleza hayo leo wakati akizunguza kwenye kikao na kamati ya siasa ya CCM kata ya Muungano kilichoketi kwa lengo la kujadili mapendekezo ya kuanzishwa kwa ujenzi wa ofisi ya CCM kata hiyo kilichofanyika shule ya msingi Mlimashabaha na kuongeza kuwa barabara hizo zinazowekewa lami zitawekwa taa za barabarabani.
"Tunaendelea kufanya kazi, Dorcas barabara inaongezwa kipande cha lami mita 200 ambacho kitafika hadi kwenye ile njia ya kwenda kwa Palanjo na mwakani tutaanza mazungumzo kwa ajili ya kuweka lami barabara ya Ngalawa kipande kilichobaki kutoka kwa mkuu wa wilaya, hospitali hadi kutokezea barabara ya Sanya Juu mita 400 tumeweka pale fedha, kuna milioni 300 tunamalizia barabara ili iunganike ya lami" amesema Rutaraka.
"Wale wanaofanya biashara barabara ya Nyerere ile barabara tayari mkandarasi amepahapatikana tunaweka lami pale mita 700 kuanzia stendi ya Bomang'ombe hadi kutokezea barabara ya Arusha, lakini pia tumepanga kuweka lami mita 200 kutoka stendi ya Rundugai kuelekea weekend"
"Vilevile milioni 300 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuweka lami barabara ya Snow view-Rundugai mita 500 na barabara ya Rundugai-TPC imeshaombewa fedha kwa ajili ya kuweka lami kilomita 26 na barabara zote hizi zinazowekwa lami zitawekewa taa, kwa hiyo usiku hakutakuwa tena na giza kwenye barabara" ameongeza Rutaraka
Kwa upande wake Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Hai Muddy Msalu akielezea utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuwaletea wananchi wa wilaya hiyo maendeleo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai