MJI wa Bomang’ombe na viunga vyake, sasa utapambwa kwa taa za barabarani, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Juma Irando, kuagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuja na zabuni ya kufunga taa za kisasa zinazotumia umeme wa jua.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Irando, ameelekeza hayo alipotembelea na kukagua matengenezo ya barabara nane zinazohusisha matengenezo ya kiwango cha changarawe na zile zinazojengwa kwa kiwango cha lami.
“TARURA (Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini), wekeni taa kama ambavyo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza. Hizi barabara zote ziwekwe taa mnapozijenga na hata zile ambazo bado hazina lami. Mmenielewa Eng. Lema? (Mhandisi Rickson Lema),”aliagiza Irando
Akifafanua zaidi kuhusu maelekezo hayo, Mhandisi Lema, amesema uwekeaji wa taa hizo utategemea bajeti zijazo, ingawa kwa bajeti ya mwaka ujao wa fedha unaoanzia Julai mwaka huu, watamega fungu la kuanza kutekeleza agizo hilo.
“Tutapunguza hata kipande kidogo cha utengenezaji wa barabara lakini tuhakikishe tunaweka na taa za barabarani. Kwa bahati mbaya bajeti ya 2022/2023 ilishapita wakati maelekezo yanatolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa” amesema Lema
“Tutaanza na barabara ya RC/Hai Hospital hadi makutano ya barabara ya Moshi Arusha, Dorkas na maeneo ya katikati ya mji.”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai