Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Hai likiongozwa na Mwenyekiti wake Edmund Rutaraka, lililofanyika leo Februari 08, 2023 limepitisha bajeti ya Halmashauri yenye thamani ya shilingi bilioni 43,365,519,984.28 kwenye mkutano maalum wa baraza la madiwani kujadili mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akisoma mpango wa bajeti hiyo mbele ya baraza la Madiwani lililofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo, mkuu wa divisheni ya mipango, takwimu na ufuatiliaji wilaya ya Hai Said Abdallah ametaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri, ruzuku toka serikali kuu na miradi ya mmaendeleo.
Katika mpango huo, halmashauri inalenga kukamilisha miradi, kuelekeza fedha kwenye miradi michache itakayotatua changamoto zilizopo kwa sasa pamoja na kukamilisha miradi ambayo inalenga kuongeza wigo wa mapato ya ndani ili kuiongezea halmashauri uwezo wa kuendelea kujitegemea.
Abdallah ametaja viapaumbele vya halmashauri kuwa ni kuhamasisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao,kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki,kuendeleza ujenzi na ukarabati wa zahanati, vituo vya afya na hosptali ya halmashauri.
“mheshimiwa mwenyekiti vipaumbele vingine ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi na sekondari,ujenzi wa vyoo shule za msingi na sekondari pamoja na kukamilisha kwa awamu miradi viporo ikiwa ni pamoja na maabara,vyumba vya madarasa na miundombinu ya kutolea huduma za afya.
Akiharisha kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri ameagiza wakuu wa idara kuhakikisha mapato yaliyokasimiwa kwenye bajaeti hiyo yanakusanywa kikamilifu kwa kutumia machine za kukusanyia fedha za mapato ya halmashauri (POS) ili kuwezesha halmashauri kutekeleza miradi na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyo pangwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai