Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, limefanya uchaguzi na kumchagua, Elingaya Massawe kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Baraza hilo limefanya uchaguzi huo leo, chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa baraza hilo Helga Mchomvu ambapo Massawe ameibuka mshindi baada ya kupata kura 15 kati ya 22 zilizopigwa na kumshinda mshindani wake Robson Kimaro ambaye amepata kura saba.
Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Joeli Nkya ambae ni diwani wa kata ya bomang,ombe ambae amemaliza muda wake.
Wakati huohuo katika kikao hicho cha baraza la madiwani mwenyekiti Helga Mchomvu amewakumbusha wananchi wilayani humo kuhifadhi chakula ili kuepuka kutokea kwa njaa hapo baadae kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha msimu uliopita wa kilimo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai