Katika picha ni Kati ya tangazo lililobandikwa kwenye Moja ya Bucha la uuzaji nyama ya Ng'ombe lililo Mjini Bomang'ombe ambalo linaonyesha kuwa kitoweo hicho kimeshuka Bei kutoka Sh.elfu 8 Hadi elfu 7 leo na hii Ni baada ya siku ya Jana Wananchi wa Wilaya ya Hai kulalamika mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa kitoweo hicho kimepanda Bei kinyume na taratibu.
Baada ya kupokea malalamiko hayo katika Mkutano wa hadhara hapo Jana April 20 2021 Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya aliagiza wafanya biashara hao ndani ya saa 24 kubadilisha Bei na kuuza kwa Shilingi elfu 6.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wafanyabiashara wameeleza kuwa kupanda kwa Bei Ni kutokana na kuadimika kwa Ng'ombe kwani wanaopatikana wanauzwa ghali hivyo kupanda kwa Bei kumetokana na kukwepa kupata hasara.
Hata hivyo leo April 21 2021 imebainika kuwa kuadimika kwa kitoweo hicho katika mji wa Bomang'ombe huku ikishuhudia baadhi ya mabucha yakiwa yamefungwa kutokana na wauzaji wa Mabucha hayo kwenda kushiriki kikao na mkuu wa Wilaya kikao kilichosababisha kufikia maafikiano yakukuza kitoweo hicho kwa sh elfu 7.