JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro kupitia kitengo cha dawati la jinsia na watoto limesema kuwa limedhirishwa na ushirikiano unaotolewa na madereva wa pikipiki za usafirishaji maarufu bodaboda katika kudhibiti matukio ya ngono za utotoni hususani kuwa walinzi wa wanafunzi.
Mwenyekiti wa dawati hilo, wilaya ya Hai Happynes Eliufoo ameyasema hayo wakati akizungumza na kwenye kipindi cha Siku Mpya cha Redio Boma Hai juu ya hali ya matukio ya mimba za utoto yanayotokea wilayani hapa.
Eliufoo amesema kundi kubwa ambalo lilikuwa likitajwa sana na kujihusisha na matukio ya ubakaji na kusababisha ujauzito lilikuwa ni la waendeshaji pikipiki (Bodaboda) jambo ambalo kwa sasa limepungua.
Amefafanua kuwa kwa sasa asilimia kubwa yawaendesha bodaboda wameacha kushiriki vitendo vya ngono na wanafunzi ambapo kwa sasa wamekuwa walinzi wa wanafunzi kwa kuwabainisha watu wanaoshiriki ngono na wanafunzi.
"Kwa muda mrefu lawama zilikuwa zinapelekwa kwa madereva wa bodaboda kushiriki ngono nakuwapa ujauzito watoto wa shule lakini sasa wanaonesha kushirikiana na jamii kuwalinda wanafunz".
Aidha Eliufoo, amewataka makundi yote ya vijana wilayani Hai kuwa mabalozi wazuri katika kuwalinda watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao na kuweza kuhudumia jamii pindi wanapohitimu elimu yao.
Nao baadhi ya wazaziMatilda Temba na Patrick Masaa wamesema kuwa ni jambo la busara kwa vijana hao kuchukua uamuzi huo mzuri na wenye tija ambao utapelekea wanafunzi kumaliza elimu bila vikwazo huku wakiwaasa wanafunzi hasa wa kike kuacha tabia ya kuwashawishi vijana na badala yake watambue thamani yao na wajibu wao.
Awali kati ya matukio matano (5) ya mimba za utotoni yaliyokuwa yakiripotiwa, matatu(3) yalikuwa yanahusisha waendesha boda boda ambao kwa sasa wameanza kushirikiana na polisi kwa kuwafichua wale wanaowakodi wakijihusisha na mahusiano na wanafunzi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai