Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ameipongeza Redio Boma Hai fm kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha umma juu ya taarifa mbalimbali za maendeleo katika wilaya ya Hai na kwingineko.
Myinga ametoa pongezi hizo alipozungumza wakati wa uzinduzi wa soko la Maiputa lililopo kata ya Masama Magharibi katika eneo la jiweni barabara ya Sanya Juu.
"Niwashukuru sana Redio Boma Hai fm mmekuwa mstari wa mbele kuhabarisha wananchi na kuhakikisha kuwa wanapata taarifa mbalimbali za maendeleo ya wilaya ya Hai na hata nje ya wilaya,nyinyi mmekuwa jicho zuri kabisa na masikio mazuri katika kuhabarisha na kuelimisha wananchi"
Aidha mkurugenzi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kufanya biashara katika soko la Maiputa ili soko hilo liweze kuwa chanzo kikubwa cha biashara na uchumi katika wilaya hiyo ambapo amewataka wenye vibanda ambavyo havijakamilika kwenye soko hilo kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Kwa upande wake Mratibu wa shughuli za uanzishwaji wa soko hilo Zephania Gunda ambaye pia ni Mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Hai ameeleza kuwa wafanyabiashara wote wa nje watakaokwenda kuchukua bidhaa katika soko hilo hawatolipa ushuru kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Januari 18, 2023 ikiwa ni ofa kwa wafanyabiashara hao ili kuwavutia wakafanye biashara kwenye soko hilo.
Mwenyekiti wa soko hilo Hossea Munuo anasema "soko limechangamka vizuri japo ni mara ya kwanza na ni siku ya kwanza lakini utafikiri soko hili lilianza mwaka mzima uliopita, tumeshagawa maeneo karibu yote kwa wafanyabiashara a soko hili litakuwa linafanyika mara 3 kwa wiki kwa maana ya jumatano, Ijumaa na Jumapili"
Mwanamke mmoja mfanyabiashara katika soko hilo akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake aanasema "soko limefurika hakuna mfano, wananchi tumeitikia tumeleta bidhaa sokoni, tuko na mkurugenzi wetu hapa kwenye uzinduzi leo"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai