Mwenyekiti wa kamati ndogo iliyoundwa na baraza la madiwani kufuatilia suala la mazingira wilayani Hai, mhe Nasibu Mndeme ameitaka bodi ya Maji Bonde la Pangani Mkoani Kilimanjaro kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi na viongozi wanaozunguka vyanzo hivyo.
Mndeme ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyolenga kukagua vyanzo vya maji katika eneo la ziwa boloti lililopo kitongoji cha Maiputa iliyowashirikisha Viongozi wa Vijiji , Watendaji na baahi ya watumishi wa bonde hilo
Amesema kundi ilo muhimu likipata elimu itasaidia kuzuia uharibufu wa mazingira unaofanyika katika maeneo mengi ya vyanzo vya maji.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Patrice Otieno Afisa Maendeleo ya jamii kutoka bonde hilo, litaweka alama za kudumu katika eneo hilo ilikufahamu mipaka halisi na kulilinda kutokana uharibifu wa shughuli za kibinadamu kutishia eneo hilo kukauka.
Otieno amesema lengo la kuweka alama hizo ni kufahamu enao la ziwa ili kulilinda na kuzuia Watu wanasogeza mipaka kila siku na kufanya shughuli mbali mbali
“Kama mlivyoona za kilimo na kuingiza mifugo hivyo lazima tutunze eneo hili ,tukiondoka hapa nani atafahamu mipaka halisi ni kweli Machi 30 mwaka huu tunaanza zoezi hilo kwa kushirikiana Viongozi wa Vijiji vinne ,vikiwamo kyuu na Mungushi na hivyo Viongozi wa vijijij hivyo na Watendaji pamoja na Wananchi wanaopakana na ziwa hilo wanatakiwa kufika "alisema
Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha Maiputa Benson Ndos, ameshukuru Bonde hilo kwa Kuona umuhimu wa kuweka vigingi ,alisema Watu wamekuwa Wakilima na kusogea kwenye ziwa kwa sababu hakuna alama.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai