Chama cha mapinduzi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimepongeza shughuli za kimaendeleo ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali huku chama hicho kikiwataka watumishi wa umma kutambua kuwa wajibu wao wa msingi ni pamoja na kuwahudumia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai Wanguba Maganda wakati chama hicho kikipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani kutoka serikalini .
Amesema kuwa baada ya chama hicho kuwaahidi wananchi katika ilani, bado CCM inalojukumu kubwa katika kusimamia utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo ikiwemo thamani ya miradi kuendana na thamani ya fedha halisi zilizotolewa.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa wilaya ya Hai Said Mtanda amesema kuwa miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa katika wilaya ya Hai huku akitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Longoi na zahanati ya Chemka vilivyogharimu milioni 900.
Aidha katika kuwaweesha wananchi kiuchumi, jumla ya shilingi milioni 193.6 zilitolewa kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye walemavu ambapo fedha hizo zilitokana na mapato ya ndani.
Naye katibu wa chama hicho Kumotola kumotola amesema kuwa baadhi ya dosari zilizojitokeza ni zile zenye kurekebishika huku pia akisema kuwa katika kipindi kijacho chama hicho hakitapokea taarifa ya mradi wowote bila ya kuwa na mchanganuo halisi wa gharama za mradi huo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai