Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimewaagiza wataalam wanaosimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha kuwa michango ya wananchi inajumuishwa kwenye thamani ya mradi hiyo ili kupata gharama ya halisi ya utekelezaji wa miradi.
Maagizo hayo yametolewa na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Hai ndugu Wang’uba Maganda wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika kata 17 za wilaya ya Hai.
Maganda amesema kutojumuisha michango ya wananchi na nguvu kazi wanayoitoa kwenye thamani ya mradi kunakatisha tamaa wachangiaji licha ya kusababisha thamani halisi ya mradi kutojulikana.
“miradi mingine ni ukamilishaji tu tayari wananchi walishajenga kwa hatua flani kama miradi imejengwa na wanachi au wadau wa maendeleo lazima thamani yake ioneshwe”amesema Maganda.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Herick Marisham ameahidi kurekebisha taarifa hizo kwa kujumuisha michango yote ya wadau wa maendeleo .
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai