Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea na utatuzi wa changamoto za wananchi ikiwemo ya kutokomeza adha ya upatikanaji wa maji katika mji wa Bomang’ombe pamoja na utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na kiwanja cha ndege cha Kia.
Rais Samia ameeleza hayo alipopita wilayani Hai na kuzungumza na wananchi katika eneo la stendi ya Sanya Bomang’ombe na kusema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 1 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji utakaokwenda kutokomeza shida ya maji wilayani Hai.
"Najua sijamaliza tatizo la maji ndani ya Bomang'ombe lakini kuna mradi mkubwa tunafanya na Halmashauri ya wilaya ya Hai, mradi wa bilioni 1 kuhakikisha kwamba tunaleta maji maeneo yaliyobaki Bomang'ombe"Rais Samia Hassan.
"Ndani ya Bomang'ombe kuna mgogoro kidogo wa ardhi unaohusisha kiwanja cha ndege, tunaushughulikia kwakupata vielelezo vya watu walio kwenye eneo kuona ikiwa wapo hapo kihalali na nani alivamia,kila mwenye haki atapata haki yake ili kumaliza mgogoro"Rais Samia Hassan
"Soko la kwa Sadala ni ndogo,najua Bomang'ombe inakama wafanyabiashara 1000 lakini soko lile ni dogo,tutajenga soko lingine kubwa eneo la Machine tools ambalo litapokea wafanyabiashara"Rais Samia Hassan
"Ninaendelea na kazi ya kutengeneza filamu itakayo onesha mazuri yalipo nchini,hii siyo ziara rasmi nilisimama tusalimiane na mjue nazijua changamoto zilizopo nitakuja ziara rasmi kuanzia mwenzi wa Novemba na Disemba najipanga kwa hilo."Rais Samia Hassan
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan ameelekea Marangu kwa ajili kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai