Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Hai mkoani Kilimanjaro,Adella Riwa amesema jamii ikifuata maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya namna Bora ya kujinga na maambukizi ya virus vya Corona itasaidia kuondoa maambuki mapya ya virus hivyo.
Ameyasema hayo leo Mei 05 ,2020 wakati akikabidhi vifaa vitakavyotumika kwa ajili kunawa mikono kwa wananchi na wafanyabiashara katika soko la kwa sadala liliko kata ya Masama kusini.
Pia ametoa rai kwa Taasisi nyingine kujitokeza na kuendelea kuungana na serikali katika kukabiliana na janga la Virusi vya Corona kwakuchangia mahitaji maalumu yanayohitajika kukabiliana na janga hilo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Hai,Yohana Sintoo amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kukabiliana na tatizo la virusi vya Corona ikizingatiwa kuwa soko hilo limekuwa likitumika na wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
"Namuelekeza Afisa Biashara kwenda kuvifunga hivi vyombo pale sokoni,na Mganga Mkuu (DMO) ahakikishe anafika kwaajili ya kuendeleza kutoa elimu yakujikinga na matumizi sahihi ya vifaa hivi." Amesema Sintoo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni mapipa matatu yalitengenezwa kisasa kwa ajili ya kunawa mikono pamoja lita 20 za sabuni vyenye thamani ya shilingi 650,000.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai