MKUU wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameagiza kuvunjwa kwa mabaraza ya ardhi ya kata tatu kutokana na kulalamikiwa na wananchi kuhujumu haki za wananchi katika kumiliki ardhi.
Mabaraza ya kata aliyoagiza kuvunjwa ndani ya saa 24 ni Machame Magharibi, Bomang'ombe na Bonden pamoja kamati za ardhi vijiji vya Mkalama , Kawaya na Rundugai.
Akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, migogoro na malalamiko ya ardhi ya wananchi wa kata 17 za wilaya hiyo.
Hadi kufikia jana alikukuwa amepokea malalamiko, migogoro na kero 266 ambazo ni kusogeza mipaka, urasimishaji makazi, fidia ya ardhi na zoezi la uwekaji alama za mipaka.
"Nakuagiza mwanasheria wa halmashauri (Henglibert Boniface) kwa kushauriana na mkurugenzi wako mtendaji ikifika kesho mniletee taarifa kuwa mmeshavunja mabaraza hayo" amesema Sabaya.
"Mabaraza haya yamekuwa yakituhumiwa kushirikiana na baadhi ya watu wenye uwezo kuhujumu haki za wananchi wanyonge kumiliki ardhi yao kwa kujali maslahi yao" alisisitiza.
"Pia nawaagiza kila kata kuitisha vikao vya maendeleo ya kata (WDC) kabla ya Machi 22 kujadili kero za ardhi kabla sijaja huko kwenye kata zenu" aliongeza Sabaya.
Kwa upande wake Mwanasheria wa halmashauri hiyo, Henglibert Boniface mesema kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa, (mamlaka ya wilaya) ya mwaka 1982, kifungu 23 zinampa mamlaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kupitia mwanasheria mamlaka ya kulivunja, kulisimamisha au kuagiza marekebisho katika mabaraza hayo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai