MKUU wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro , Lengai Ole Sabaya amepongeza ushirikano ulipo kati wakuu wa idara na watumishi wa idara zao hali iliyopelekea kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Ole Sabaya ametoa pongezi hizo wakati akitoa salamu za Rais kwa watumishi wa Halmashauri na kusema kuwa wamekuwa na ushirikiano bila kujali tofauti zao za madaraja hali ambayo imefanikisha kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuendelea kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Amesema serikali ya awamu ya tano imesisitiza umuhimu wa ushirikano miongoni mwa watumishi na kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuboresha ukusanyaji wa kodi za serikali ambapo watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai wameelewa kasi ya Rais Dkt John Magufuli .
"Napongeza sana ushirikiano ulipo kwenu watumishi wa halmashauri hii, mmefanya kazi nzuri na imenipa sifa kwa Rais kwa kusimamia mapato na halmashauri yetu kuwa juu, na sio kwa mapato tu hata mwaka uliopita tuliweza kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na miradi bora katika mbio za mwenge wa uhuru; nawapongeza sana" Amesema Ole Sabaya.
"Mkuu wa idara ya fedha umesimama katika nafasi yako kwa kushauri vizuri namna Bora ya ukusanyaji wa mapato yetu; hongera sana kwa hilo"
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka watumishi hao kuhakikisha kila idara inakuwa na mpango mkakati wake utakaobainisha jinsi ya kupata mapato kupitia vyanzo vilivyoko kwenye maeneo ya kazi.
Hata hivyo , Ole Sabaya amesema kuwa mafanikio yote hayo yamechangiwa na nidhamu iliyojengeka kwa watumishi wa umma pamoja na kuwa na uzalendo chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano .
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai