Serikali wilayani Hai imewataka viongozi wa vijiji na kata kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo ili iweze kukamilika kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa ametoa agizo wakati alipotembelea miradi mbalimbali ya elimu katika kata ya Weruweru na Mnadani pamoja na kuzungumza na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yao.
Amesema Serikali imekuwa ikitumia fedha kutekeleza miradi kwa lengo lakini badhi viongozi wameshindwa kusimamia kwa kina jambo ambalo limesabisha miradi kukamilika kwa viwango vya chini .
Amesema viongozi wa maeneo inapotekelezwa miradi wanapaswa kutambua thamani na mda wa kukamilika ili iweze kukamilika kwa viwango vilivyokusudiwa ili iweze kudumu na kuhudumia kwa mda muafaka.
Hata hivyo, Mkalipa amewata wale wote wanaondaa malipo kwa ajili ya wakandarasi kuwalipa kwa wakati ili samahani ya fedha ya miradi iweze kuonekana.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai