Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Hassan Bomboko amewasihi wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftri la kudumu la mpiga kura
Akitoa taarifa kwa Umma kuhusu zoezi hilo Bomboko amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuahikiki taarifa zao na pia kwa wale waliojiandikisha basi wajitokeze kuakiki taarifa zao kwani ndio msingi wa uchaguzi huru na haki
Hata hivyo Bomboko amewataka viongozi wa dini kuwaeleza waumini wao kuhusu umuhimu wa jambo hili na amewaomba wawasihi waumini wao kujitokeza kujiandikisha
Kwa upande mwingine Bomboko ameeleza umuhimu wa kupiga kura kwa kila mwananchi kwa itikadi yake ili kumchagua kiongozi bora na kuachana na upotoshaji wa baadhi ya watu wanaopinga zoezi hilo
Zoezi la uboreshaji wa daftrai la kudumu la mpiga kura awamu ya pili wilayani Hai limeanza leo tarehe Mei 16 hadi Mei 22, 2025.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai