Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemtaka mwekezaji wa shamba la maua la Mkufi; Bondeni Flowers Limited kuanza kuwanunulia wafanyakazi wa shamba hilo vifaa vya kazi ndani ya siku saba.
“Nataka tuanze na buti, nimekupunguzia moja ila nataka tupeane muda wa kukamilisha zoezi hilo. Nakupa siku saba hadi ifikapo tarehe 22 nikute watu wote wana buti hapa”. Amesisitiza Sabaya.
Akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa shamba hilo, Sabaya amesema ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wananchi wake wanafanya kazi katika hali ya usalama.
“Mimi nina kazi kuu mbili; ya kuhakikisha kodi ya Serikali inapatikana na kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge ambao Rais wan chi hii Dkt. John Pombe Magufuli ametuagiza kuwapunguzia kero na kuboresha maisha yao”. Amesema Sabaya.
Aidha Sabaya amewataka watanzania waliopewa kazi za kiutawala kwenye shamba hilo kutojisahau na kuwatenga wananchi wenzao na kusababisha wakandamizwe na kunyimwa haki zao.
Pamoja na hayo amewashauri wamiliki wa shamba hilo kutafuta menejimenti itakayowasaidia kuwa daraja kati ya uongozi na wafanyakazi ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na kukosekana kwa mawasiliano kati yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai