Diwani wa kata ya Machame Magharibi Mhe.Martin Munisi amewataka wananchi wa Kijiji Cha Nronga kuacha tabia ya unywaji wa pombe kupitiliza hasa wakati wa kazi kwani inasababisha vijana kutojishughulisha katika ufanyaji wa kazi na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwwmo uwizi.
Hayo yamesemwa katika kikao Cha diwani na wanachi katika Kijiji Cha Nronga kata ya Machame Magharibi.
Aidha diwani Munisi amewataka pia wananchi kukemea vitendo vya kikatili kwa watoto na kuwataka kutolea taarifa vitendo vya kikatili katika kituo Cha polisi pindi wanapoona matukio ya kihalifu.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji Cha kata hiyo amewahasa wananchi wenzake kuonyesha ushirikiano kwa serikali hususani jeshi la pindi wanapohitaji kumkamata mwahalifu kwa ajili ya uchuguzi.
Naye Polisi kata Glory John amewataka wananchi kufanya kazi halali kwa kujitafutia kipato kwa njia iliyo halali.
Afande Glory amewataka wazazi kuacha kupokea zawadi ama fedha kutoka kwa watoto wao bila kufahamu kazi au shughuli anayofanya ya kujipatia kipato.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai