Diwani wa kata ya Masama kusini Cedrick Pangani amezikumbuka kaya masikini katika kijiji cha Mkombozi kilichopo kata hiyo kwa kutoa msaada wa vyakula, nguo pamoja na vinywaji vyenye thamani ya shilingi million 1 kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya akieleza kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mwaka jana niliweza kupeleka katika kijiji cha kwa Sadala na mwaka huu tumeona tulete hapa kijiji cha Mkombozi na Mungu akijalia mwaka ujao tutapeleka kijiji cha Kware, lakini pia tunamuunga mkono Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ambapo jana(23 Des 2021) yeye ametoa na akishatoa yeye sisi kwetu ni maagizo ambao tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi”
Mwenyekiti wa kitongoji cha Korongoni kilichopo kijiji cha Mkombozi Abtwalib Juma amemshukuru diwani huyo kwa msaada aliotoa kwa wananchi wa kitongoji hicho ambao utasaidia wananchi hao kusherehekea sikukuu hiyo kama wananchi wengine.
Wananchi hao waliopata msaada huo wamemshukuru diwani Pangani kwa upendo anaoendelea kuonesha kwa wananchi wa kata hiyo ambapo wameeleza kuwa hapo awali hakuja wahi kutokea diwani aliyekaribu na wananchi wake ukilinganisha na diwani Pangani
“Mimi kama mimi kwanza kabisa nampongeza diwani wetu, tangu tumepata madiwani hatujawahi kupata diwani kama huyu huwa tunachagua diwani lakini tunakuja kumuona kipindi cha kugombea tena”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai