Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe.William Ole Nasha amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa Elimu ya ufundi kuelekea Tanzania ya viwanda imeendelea kufanya uwekezaji katika vyuo vya ufundi kwa kuongeza udahili na ubora katika elimu ya ufundi.
Akizindua kituo cha mafunzo ya kufua umeme kwa kutumia Nguvu ya maji kilichopo Kikuletwa Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe.Ole Nasha amesema kutokana na uwekezaji unaoendelea serikali imeendelea na ujenzi wa vyuo vipya vya ufundi stadi 43.
Aidha amesema kuwa kitokana na uwekezaji huo idadi ya wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya ufunfi imeongezeka kutoka elfu 30 kwa mwaka 2015 hadi kufikia 151969 mwaka 2019 ambapo weendelea kuhakikisha fani zinazotolewa kayika vyuo vya ufundi zinaendana na get mahitaji halisi ya soko.
Ameongeza kuwa mkakati huo unaohusisha miradi mingine umefadhiliwa na serikali ya Norway kwa gharama ya shilingi bilioni 8.3 ili kuwezesha serikali ya awamu ya tano kufikia dira ya maendeleo ya taifa inayolenga kujenga uchumi imara na kuondoa umaskini na kuleta hali bora ya maisha kwa wananchi.
Sambamba na hayo amesema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani 3.9 utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2115 za umeme,kiasi ambacho ni kikubwa kuliko umeme unaozalishwa kwa sasa nchini ambapo ameitaka bodi na uongozi wa kituo hicho kuhakikisha mitaala ya mafunzo inahuishwa mara kwa mara ili kuendana na majitaji ya wakati husika.
Vilevile ameongeza kuwa uzalishaji wa kituo hicho umelenga kuhakikisha wataalamu hasa mafundi stadi na mafundi sanifu wanapatikana ili kuongeza ufuaji wa umem kutoka vyamzo vidohovidogo na vikubwa vya maji ambapo lengo ni kutoa mafunzo kwa vitendo na kufanya tafiti juu ya nishati jadidifu ikiwemo uzalishajo umeme kutokana na nguvu ya maji.
Pamoja na hayo amesema serikali imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa elimu ya ufundi Afrika Mashariki unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 75 ambapo umelenga kuleta mapinduzi katika elimi ya ufundi nchini kwa kuvijengea vyuo uwezo ili viweze kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi stahiki wa kuwawezesha kujiajiri.
Awali akizungumza mbele ya Naibu waziri hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amesema kama serikali watailinda miundombinu itakayo tengenezwa kwa kiwashirikisha viongozi wa kijiji waliopo katika ulinzi huo.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt. Masudi Senzia amesema kuwa kituo hicho ni zao la mradi wa ushirikiano kati ya Serikali na Norway kupitia ubalozi wake nchini Tanzania na Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya fedha na mipango ambapo mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2014 na ukomo wake kufikia Desemba 2019.
Akitoa historia ya eneo la mradi huo Dkt.Masudi amesema kuwa baada ya shirika la umeme nchini kumilikishwa eneo hilo na serikali ya kikoloni ya wajerumani uwezo wa uzalishaji umeme ulipungua kutokana na uchakavu wa mitambo na kupelekea kusimama kwa uzalishaji umeme mnamo mwaka 1988 kwa kuharibika kwa mitambo yote na gharama.
Amesema ili kuongeza uwezo wanataaluma 32 wa chuo cha ugundi Arusha katika kuzalisha umeme ambapo chuo kimetayarisja mitaala miwili ya kufundisha iliyopata kibali cha VETA na NACTE kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Afisa mwandamizi wa elimi kutoka Benki ya Dunia Ndg.Nkahiga Mathus Kaboko ameipongeza serikali kwa juhudi inazozifanya ya kuhakikisha wanazalisha nguvu kazi ambayo ina umahiri ambapo kwa kutambua mchango huo Benki ya Dunia imeamua kuja na wazo la kusaidia serikali katika kuanzisha kituo hicho.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai