Mwenyekiti wa kamati ya Sensa wilaya ya Hai ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Juma Irando amewataka Makarani wa Sensa wilayani humo kwenda kuifanya kazi ya kitakwimu kwa weledi na kuzingatia kiapo walichoapa.
Makarani wa Sensa wilaya ya Hai wapatao 1091 wameapishwa leo na hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilaya hiyo Julieth Mawole kwa ajili ya kwenda kuanza rasmi zoezi hilo nyeti la kitaifa Agosti 23 2022.
Aidha Mwenyekiti huyo wa kamati ya Sensa akifunga mafunzo ya Makarani wa Sensa kwenye ukumbi wa Mong'are wilayani humo, amewapongeza Makarani hao kwa kuhudhuria mafunzo kikamilifu kwa siku zote 16.
"Nawapongeza kwa siku zote 16 ambazo mmehudhuria mafunzo haya na bahati nzuri sijapata taarifa juu ya changamoto yoyote kwa hiyo ninaamini kwamba mmefanya vizuri, pia mkafanye kwa weledi kazi hii kwa kuwa mmeaminiwa na nyie mkaaminike"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai