Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utahusisha vijiji,vitongoji, mitaa na wajumbe,zinatarajiwa kutolewa hapo kesho Octoba 29.
Wakati zoezi hilo likianza wanawake kote nchini wenye sifa zilizoainishwa na tume ya uchaguzi wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi katika maeneo yao.
Ushauri huo umetolewa na Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Hai Juma Masatu mapema leo akizungumza na Radio Boma Hai Fm ofisini kwake, ambapo amesema kuwa watu wote wenye sifa na wameidhinishwa na vyama vyao wanatakiwa kujitokeza kuchukua fomu kabla ya muda kumalizika.
Mapema leo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, ametangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kuchukua na kurejesha form za kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi za vijiji, Mitaa, Vitongoji na wajumbe, kwa ajili ya uchaguzi serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Aidha amesema maandalizi yote kwa ajili ya zoezi hilo yamekamilika, na kuwataka watu wote wazingatie kanuni na taratibu wakati wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa form hizo na kuwataka wasimamizi na wasaidizi wao kusimamia kikamilifu zoezi hilo.
Katika hatua nyingine amewataka Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao ndio wasimamizi wa ulinzi na usalama kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama unakuwepo katika mda wote wa zoezi hilo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai