Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Hai Yohana Sintoo amewataka wataalamu wanaoshiriki zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Wilaya ya Hai kutekeleza majukumu yao huku wakizingatia maelekezo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Sintoo ametoa angalizo hilo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa saidizi ngazi ya kata pamoja na opareta wa mashine za kuandikishia (BVR machine) na waandishi wasaidizi ngazi ya kituo.
Amewataka wataalamu hao kuwahudumia wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa ambao watafika kwenye vituo vyao huku wakiendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona pamoja na kuwaelekeza na kufanikisha zoezi la kujikinga ikiwemo kuweka maji tiririka na sabuni na kuwaelekeza kukaa umbali wa mita mbili kuoka mtu mmoja hadi mwingine.
Zoezi la kuboresha Daftari la Wapiga Kura katika wilaya ya Hai linafanyika kwa siku tatu kuanzia Ijumaa tarehe 17/04/2020 hadi Jjumapili tarehe 19/04/2020 likihusisha kata 17 za wilaya hiyo na kuwapa fursa wakazi wake kurekebisha taarifa zao zenye makosa, kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama na kubadilisha makazi pamoja na kutoa kitambulisho kipya kwa wapiga kura waiopoteza au kadi zao kuharibika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai