Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan pamoja na serikali yake kwa kutoa fedha za kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo ikiwemo shule na vituo vya afya katika wilaya ya Hai.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya fedha,Uongozi na Mipango Rutaraka pia ametoa pongezi kwa viongozi wa miradi wakiwemo madiwani, na watumishi wa halmashauri kwa kupokea fedha zilizotolewa na Rais na kuzifanyia kazi ipasavyo na kukamilisha miradi iliyokusudiwa na serikali.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mganga Mkuu katika ziara hiyo Innocent Mombeki ambaye Afisa Lishe amesema kuwa miradi yote ya afya imekamilika kwa asilimia kubwa na imefanyika kikamilifu kwa fedha za mapato ya ndani na miradi hiyo imefika ukingoni ambayo ni kituo cha afya Longoi,masama kati, na kituo cha afya kisiki.
Naye Mkurungezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dions Mnyinga amewataka wasimamizi wa miradi ngazi ya vituo kuendelea kusimamia vema miradi hiyo ili huduma iliyo lengwa kwa wananchi itolewe kwa wakati.
Kamati hiyo leo imetembelea na kukagua ujenzi wa madarasa 5 na choo cha matundu sita yenye tahamani ya shilingi 137,500,000 katika shule ya sekondari Lyamungo na ujenzi wa jengo la wagonjwa wan je (OPD) katika kituo cha Afya Masama Kati unaotarajia kugarimu kiasi cha shilingi 209,000,000.
Miradi mingine ni ujenzi wa njia za kupitishia wagonjwa ,kichomea taka na jengo la kufulia inayotarajiwa kugarimu shilingi 139,000.000 na ujenzi madarasa mawili katika shule ya Waramu kwa gharama ya shilingi 50,000,000.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai