Katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wella ameipongeza kamati ya Afya ya msingi ya wilaya hiyo kwa namna walivyotekeleza kwa ufanisi majukumu waliyopewa ya kuhakikisha zoezi la chanjo linafikiwa kulingana na malengo yaliyopo.
Ameyasema hayo Julai 21 2022 wakati akizungumza kwenye kikao chenye lengo la kuonyesha namna kampeni ya chanjo ya polio ilivyofanikiwa sambamba na Mwenendo wa chanjo ya uviko 19 kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Naye Mratibu wa chanjo wilaya ya Hai Alice Mchelo ameeleza kuwa kampeni ya chanjo ya polio kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano wilayani humo imefanikiwa kwa asilimia kubwa ukilinganisha na malengo waliyopewa.
“Lengo lilikuwa ni kuchanja Watoto 35,992 ambao ni watoto wote waliokuwa chini ya umri wa miaka mitano katika wilaya yetu ya Hai, lakini tumefanikiwa kuwafikia Watoto 38,928 ambayo ni sawa na asilimia 108.16 ya lengo tulilopewa” amesema mratibu huyo wa chanjo.
Wilaya ya Hai ni moja ya wilaya zilizotekeleza kampeni ya chanjo ya matone ya polio ili kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa awamu ya pili iliyofanyika kuanzia Mei 18 -21, 2022.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai