Halmashauri ya wilaya ya Hai imepokea jumla ya fedha shilingi bilioni 1.9 za miradi ya maendeleo Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kutoka serikali kuu, pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Afya.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Afya mbele ya Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Juma Irando amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa kuiwezesha wilaya hiyo katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za kijamii na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Irando ameeleza kuwa wilaya hiyo ina hospitali mbili kwa ngazi ya wilaya ambapo ni hospitali ya wilaya na Hospitali ya Machame inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), vituo 8 kati ya hivyo 7 zinamilikiwa na Serikali na 1 cha mtu binafsi, huku Zahanati 57 zinamilikiwa na mashirika 23 na 29 zinamilikiwa na Serikali.
“Katika mwaka wa fedha 2020/21 kwenye masuala ya kinga, tiba na miundombinu, Halmashauri kupitia Sekta ya Afya imewapatia wananchi 144,128 wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19 kati ya lengo na wananchi 158,673 sawa na 90.8%” amesema Irando
Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameitaka divisheni ya Afya na viongozi wa wilaya hiyo kushirikiana ili kutimiza lengo la kutoa huduma stahiki za Afya kwa wananchi kwa kuzingatia kanuni, sheria na maadili.
“Napenda kuwapongeza Mkuu wa Wilaya (Juma Irando) na mbunge wa jimbo la Hai (Saashisha Mafuwe) kwa kuonesha ushirikiano kwenye Idara ya Afya pamoja na mapokezi mazuri, pia mjitahidi katika masuala ya bima ya afya, mkifanya kitu kizuri muache taarifa hapa hata mtu akija kulalamika kuwepo na taarifa kama ushahidi”
Naibu waziri Wa Afya Dkt. Godwin Mollel katika ziara yake wilayani Hai ametembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha Afya unaoendelea katika kata ya Masama kati ambapo hadi sasa imepokea fedha shilingi milioni 20 kati ya milioni 50 za makusanyo ya ndani ya halmashauri zilizotengwa na hadi kukamilika kituo hicho kitagharimu zaidi ya mil 700.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai