Halmashauri ya wilaya ya Ha imepokea vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wa darasa la awali vitakavyogaiwa Kwa shule 14.
Akikabidhi vifaa hivyo Kwa waalimu wakuu Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Ali God amewataka waalimu waliokabidhiwa Vifaa hivyo kuvisimamia na kuhakikisha kuwa vunafanya kazi ilivyokusudiwa.
God pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta vifaa hivyo vitakavyo ongeza ufanisi kwenye kufundishia.
Kwa upande wake Mwalimu Bindael Eliurio Munisi was shule ya msingi Nkwarungo amesema vifaa hivyo vitawawezesha watoto katika masomo yao.
Aidha amesema wingi wa vifaa hivyo vitawawezesha walimu kufundisha kwa vitendo jambo ambalo litasaidia wanafunzi kuelewa kwa wapesi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai