Serikali wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imeipongeza idara ya Afya wilayani humo kwa juhudi inazoendelea kuzifanya katika mapambano dhidi ya homa Kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Kutokana na Juhudi hizo zimesababisha wilaya ya Hai kutokuwa na madhara yoyote makubwa yanayosababishwa na Virusi vya Corona.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameyasema hayo wakati akizungumza na wataalamu wa Afya, viongozi wa Dini pamoja na wakuu wa Shule 10 za Sekondari zenye Kidato cha Sita.
Ole Sabaya amesema idara ya Afya imefanya Kazi Kubwa katika kupambana na janga la COVID-19 Kwa kuhakikisha kuwa wanatoa elimu bora kwa wananchi namna ya kupambana na Janga hilo.
Katika hatua nyingine Sabaya amewataka wakuu wa Shule kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaripoti Shuleni kwa muda uliopangwa na serikali Juni 1 2020 ili waweze kujiandaa na mitihani ya kuhitimu kidato cha sita inayotarajiwa kuanza June 29 mwaka huu.
Aidha Sabaya amesisitiza kuwa kwa wanafunzi ambao watashindwa kuripoti shuleni kwa tarehe husika wachukuliwe hatua.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai