Halmashauri ya Wilaya ya Hai inaendelea kuchukua hatua za kujikinga na kuwalinda wananchi wake dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mafua inayosababishwa na virusi vya corona kwa kutoa elimu kwa wananchi wake kuhusu namna bora za kujikinga na kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Yohana Sintoo akizungumza baada ya kamati ya kuhamasisha na kuzuia Virusi vya Corona wilayani hapo kufanya ziara katika Soko la Kwasadala kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.
Amesema kuwa hivi sasa wamekuwa wakitembela katika masoko mbalimbali yaliyopo katika wilaya hiyo ili kujionea hali halisi kwenye maeneo hayo ya mikusanyiko na kujua ni hatua gani zitafaa kuchukuliwa.
Sintoo amesema kuwa baada ya kuona changamoto zilizopo kwenye masoko hayo ikiwa ni pamoja na eneo la kunawa mikono kukosekana hivi sasa halmashauri hiyo itaweka matenk ya maji kwenye kila mlango wa kuingia na kutoka katika masoko hayo hususani soko la kwasadala linalokusanya wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia amesema Wilaya inafuatilia kwa ukaribu wageni wanaoingia kutoka maeneo mbalimbali na nje ya nchi na kwamba tayari amekwishaagiza Watendaji wa Kata wakishiriana na Watendaji wa Vijiji kuhakikisha kuwa wanapata taarifa za wageni hao na kwamba katika taarifa ambazo tayari wamekwishazipata kutoka kwa wananchi juu ya wageni walioingia kutoka Nje ya Nchi tayari hatua zimeshachukuliwa ikiwa ni kuwapeleka Karantini kwa siku 14.
Aidha amewataka wafanya biashara wote Kuweka vyombo vya kunawia maji yanayotirika na Sabuni pamoja na vitakasa mikono kwenye maeneo yao ya biashara na kuhakikisha kuwa kila anaefika maeneo yao ananawa mikono yake wakati wakuingia na wa kutoka.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai