Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amekabidhi mifuko 20 ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tatu kwa viongozi wa kata ya Mnadani kwa ajili ya ujenzi wa choo cha walimu kwenye shule ya msingi Mijongweni.
Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji leo, Sintoo amesema kuwa imetokana na ahadi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr. Hatibu Kazungu ambaye aliahidi kuchangia kwa ajili ya kuanza ujenzi wa choo hicho.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mnadani Sembuli Mkilaha amemshukuru Katibu Tawala wa mkoa kwa kutimiza ahadi yake ya kuchangia saruji hiyo kwa ajili ya ujenzi ambao utatatua kero ya kukosekana kwa choo cha walimu kwani hadi sasa walimu hao wanatumia choo cha zahanati ilipo eneo la jirani na shule hiyo.
Awali akizungumzia ujenzi wa choo hicho Mkilaha amesema kuwa ujenzi unategemea kukamilika ndani ya miezi 6 na utagharimu jumla ya shilingi milioni 16.
Naye mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Omari Mgalla ameshukuru kwa mchango huo na kuahidi utaelekezwa katika ujenzi wa choo kama ilivyokusudiwa.
Kukosekana kwa choo cha walimu shuleni hapo kumesababisha walimu wa shule hiyo kujisaidia katika choo cha zahanati jirani na shule hiyo zaidi ya miaka 10.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai