Baraza la Madiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro limeazimia kujitolea nguvukazi kwa ajili ya kusaidia maeneo yaliyopata maafa kutokana na uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha hivi karibuni na kuathiri zaidi ukanda wa chini wilayani humo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Helga Mchomvu wakati wa kikao cha kawaida cha baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri na kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya wananchi.
Amesema kuwa maafa yaliyotokea na kusababisha athari ikiwemo uharibifu wa miundombinu ya barabara, huku wananchi wakihimizwa kujitolea nguvu kazi za kuchimba visima na mabwawa kwa ajili ya kuhifadhi maji na yatakayotumiwa kuendesha kilimo cha kisasa.
“Kuna maeneo yameathirika sana hasa ukanda wa chini ikiwemo Kata ya Kia kama ilivyosikika kwenye taarifa za kata; kwa upande wa uharibifu wa barabara tunaendelea kushirikiana na TARURA kutambua na kurekebisha ” amesema Mchomvu.
“Madiwani wanaendelea kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kuangalia maeneo wanayoweza kuyafanyia kazi kwa kutumia nguvu ya wananchi” Ameongeza Mchomvu.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyi Elia Machange amebainisha kuwa sehemu kubwa ambayo ilipata maafa ni katika ukanda wa tambarare hasa katika kata ya KIA ambapo Halmashauri ilichangia vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni mbili ili kuwasaidia wananchi kumudu maisha katika wakati huu.
“Watu 102 kwenye kaya 21 wameathirika na mafuriko na hatua kadhaa zimechukuliwa; kwanza alitembelea Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye alitoa msaada akishirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) na halmashauri imepeleka msaada kwa wananchi hao.”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai