• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Accounts and Finance
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Halmashauri ya Hai Yaendelea Kuimarisha Sekta ya Elimu

Imetumwa: October 1st, 2020

Wilaya ya Hai inaendelea kutekeleza mikakati ya kuimarisha kiwango cha ufaulu kwenye mitihani ya kitaifa kwa kuimarisha sekta ya elimu katika wilaya hiyo.

Kwa miaka minne mfululizo wilaya hiyo imefanikiwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa ngazi ya elimu ya msingi na sekondari kwa upande wa kidato cha nne pamoja na kidato cha sita.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Yohana Sintoo wakati akizungumza katika harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara na ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Mailisita iliyopo Kata ya Mnadani wilayani humo.

“Katika wilaya ya Hai elimu imeendelea kufanya vizuri sana, tumeendelea kufanya vizuri katika Taifa hili ambapo tumefanikiwa kuwa katika Halmashauri kumi bora kwa mfululizo wa miaka minne hadi leo” amesema Sintoo.

Akizungumzia mipango ya Serikali kuimarisha elimu; Sintoo amesema kuwa Halmashauri imepokea zaidi ya milioni 900 kwa ajili ya kukarabati shule ya sekondari ya wasichana Machame, huku zaidi ya milioni 800 zikitolewa  kukarabati  shule ya sekondari Lyamungo na shilingi milioni 64 zikipelekwa katika shule ya sekondari Longoi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu.

Awali akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi; Mkuu wa Shule ya Sekondari Mailisita;  Josina Misago amesema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa hali inayopelekea wanafunzi zaidi ya sabini kusoma katika chumba kimoja cha darasa huku wengine wakilazimika kwenda kusoma katika chumba cha maabara ambacho hakijakamilika ujenzi wake.

“Changamoto ni uhaba wa madarasa ukilinganisha kwamba darasa linakaa wanafunzi 40, sisi kwetu wanafika 50 hadi 70 kwahiyo hiyo inatupa adha kubwa hasa katika usimamiaji wa taaluma darasani mwalimu inakuwa nivigumu kufuatilia watoto.”amesema

Kuhusu maabara amesema kuwa ukosefu wake umesababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa masomo ya sayansi huku wanafunzi wengi wakishindwa kuchagua mchepuo wa Sayansi hivyo ameiomba serikali na wadau wa elimu nchini kujitokeza kuchangia kukamilisha ujenzi wa maabara pamoja na madarasa ili kuondoa adha hiyo.

Hata hivyo katika harambee hiyo ambayo iliendehswa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yohana Sintoo na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu Kilimanjaro iliwafanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Milioni 65 kati ya milioni 115 zilizokadiriwa kukusanywa huku ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ikichangia Milioni 25.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA YA UDEREVA March 28, 2025
  • TANGAZO LA MKOPO KWA WATUMISHI December 20, 2024
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIMBO LA HAI 2024 December 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA October 29, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Shule Ya Msingi Nguzo Nne Yashika Nafasi Ya Pili Kwa Usafi

    April 09, 2025
  • Wananchi Wa Hai Wapo Tayari Kwa Uchuguzi

    April 05, 2025
  • Wananchi Wa Hai Wapo Tayari Kwa Uchuguzi

    April 05, 2025
  • Mkuu Wa Wilaya Ya Hai Ameongeza Anna Boniface

    March 24, 2025
  • Ona Yote

Video

UGAWAJI WA PIKIPIKI WILAYA YA HAI
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • BARUA PEPE YA MALALAMIKO
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai

    Simu: 0754553560

    Simu ya Mkononi: 0754553560

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai