Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai amemtaka Mkuu wa Idara ya Fedha kuweka mkakati thabiti wa kukusanya mapato kwenye mwaka mpya wa fedha unaoanza mwezi Julai 2020.
Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha watumishi wa makao makuu ya halmashauri hiyo mapema leo 13/07/2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa halamsahuri hiyo Sintoo amesema ipo haja ya kuongeza kasi ya kukusanya mapato tangu mwanzo wa mwaka.
“Mkuu wa Idara ya fedha andaa mkakati wa kukusanya mapato na ikiwezekana tuongeze kiwango kutoka asilimia 25 kwa robo mwaka hadi 28 ili kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya ukusanyaji ifikapo mwisho wa mwaka.” Amesema Sintoo.
Aidha Sintoo amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuongeza nguvu katika kuwafikishia wananchi vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili kuwapunguzia kero na kuwafanya wajasiriamali kuendesha biashara zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.
Akiwasilisha mwenendo wa zoezi la kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo; Afisa Biashara Wilaya ya Hai Ernest Mhapa amesema kuwa halamashauri hiyo hadi sasa imegawa vitambulisho 1678.
Amewakumbusha watumishi ambao tayari wamegawa vitambulisho hivyo kuwa wanatakiwa kuwasilisha taarifa za fomu walizojaza taarifa za wafanya biashara wadogo kwani kukaa na fomu kabla hazijaingizwa kwenye mfumo kunachangia kuifanya halamashauri kubaki nyumba ikilinganishwa na halmashauri nyingine za Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kila siku ya Jumatatu saa moja na nusu hadi saa mbili kamili asubuhi ambapo watumishi wanaelezea utekelezaji wa kazi kwa wiki iliyokwisha na mipango ya kazi kwa wiki inayoanza ili kuweka uelewa wa pamoja wa kazi zinazotekelezwa katika halmashauri hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai