HALMASHAURI ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kupata hati safi kutokana na utendaji wake wa ukusanyaji mapato kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Helga Mchomvu katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ambapo amesema kuwa Halmashauri imepata hati safi kutokana na watendaji wake na madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano katika suala zima la kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kiwango kinachotakiwa.
Aidha amewataka watumishi kufuata misingi imara itakayowawezesha kudhibiti mapato na matumizi ya Halmashauri kwa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma kama kuchelewa kuwasilisha mahesabu kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) , kuchelewa kuwasilisha taarifa za matumizi bila ya kuwa na viambatanishi vya malipo.
Mchomvu amesema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwashauri madiwani kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kuweza kudhibiti mapato na matumizi ya Halmashuari na kuweza kufanya vizuri zaidi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewahimiza madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka kuwatendea haki wananchi ambao wamewachagua kwa kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi pamoja na kutatua kero zinazowakabili.
Katika hatua nyingine madiwani wamekubaliana kuendelea kutumika kwa soko la walaji la Bomangombe kama ilivyokuwa likitumika wakati utaratibu wa kuanzishwa kwa soko la Gezaulole ukiendelea.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai