Halmashauri ya wilaya ya Hai imepongezwa kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Nurdin Babu katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai uliojadili taarifa za Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Pamoja na pongezi hizo Babu pia amewapongeza kwa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na kusema kuwa ni wajibu wake kuelekeza viongozi mahala palipo na fedha kuchukua ili kuweza kufikia malengo.
Kwa upande wake kaimu katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa,Piasano Kilumbi amesema katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30,2024 halmashauri ya wilaya ya Hai ilikuwa ni asilimia 105 katika ukusanyaji wa mapato.
Pia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai kuhakikisha mapato yatokanayo na stendi yanathibitiwa vizuri pamoja na kutazama bajeti ya mwaka 2025/2026 kukuzwa kutokana na wigo wa vyanzo vya mapato vilivyopo.
Naye mkuu wa wilaya ya Hai Mheshimiwa Amiri Mkalipa amesema uwepo wa Timu ya wataalam Imara,madiwani makini na kamati ya Ulinzi na Usalama bora watu imewezesha halmashauri kuvuka lengo la makusanyao.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Ndugu ,Dionis Mnyiga amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuisadia halmashauri ili ipate malipo ya Bima ya afya iliyoboreshwa ICHF Kwa wakati kwakuwa fedha hizo zinatengewa bajeti.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai