Jumla ya vikundi 17 vya wanawake, vijana na walemavu wilayani Hai vimewezeshwa na halmashauri ya wilaya hiyo shilingi milioni 129 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo katika mwaka wa fedha 2020/21.
Zoezi la kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa vikundi hivyo limefanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na kukabidhiwa na Mbunge Wa Jimbo hilo Saashisha Mafuwe.
Akikabidhi hundi hiyo Mafuwe amesema kuwa Mkopo huo usiyokuwa na riba ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imelenga kuwakwamua kiuchumi Wananchi wake ambapo Ni wajibu uliowekwa na sheria kwa Serikali za Mitaa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa.
Amesema ili kuwa na ufanisi zaidi kwenye vikundi hivyo baada ya kupata mikopo ataweka utaratibu wa kuvitembelea ili kuona wanafanya nini na pia kuchukua hatua kwa wasiotaka kurejesha marejesho ya Mkopo huo na kwamba serikali haitakubaliana na kikundi chochote kitakachotumia fedha hizo kinyume na utaratibu.
Aidha amesema kuwa kikundi kitakacho fanya marejesho ya Mkopo huo kwa wakati unatakiwa ndicho kitakacho pewa kipaumbele kwenye Mkopo ujao.
"Tunatamani fedha hizi zitumike kwenu, mrejeshe kwa wakati,lakini ninachowahakikishia wote mtarejesha naninaimani, namsipo rejesha kwa hiari tutawalazimisha".amesema Mhe.Saashisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha kuwa wanawatembelea na kuwasikiliza akiña mama wote wenye uhitaji wa mikopo na waliopo kwenye vikundi vyote kuhakikisha watapatiwa mikopo.
Aidha Sintoo amewataka wawatembelee walionufaika na mikopo hiyo ili kuona kama wanatekeleza majukumu waliyoombea mkopo na kuwasaidia iwapo watakutana na changamoto.
Mikopo inayotolewa na Halmashauri za Wilaya chini ya sheria ya fedha ya serikali za mitaa sura 290 inasema kuwa Katika kutekeleza wajibu wa serikali za mitaa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato Mkurugenzi atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa inatenga asilimia kumi za mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo na mikopo inatolewa kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Vikundi vilivyokopeshwa vinarejesha mikopo kwa wakati.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai