Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imetoa mkopo wa jumla ya shilingi milioni 94 na laki 9 na kuvikopesha vikundi 9 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi hundi yenye thamani ya fedha hiyo, mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafue amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia watanzania hasa kwenye mikopo isiyokuwa na riba.
Saashisha amesema kuwa mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya makusanyo ya ndani ni ya kisheria hivyo vikundi hivyo vinapaswa kurejesha kwa wakati ili wengine waweze kupata mikopo hiyo kama ambavyo wao walivyopewa.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amesema kuwa lengo la kutoa mikopo hiyo ni kuimarisha uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo na kuongeza kuwa hali ya urejeshwaji ni nzuri kwa vikundi ambavyo vimekuwa vikikopeshwa mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
Kwa upande wao wanufaika wa mkopo huo waliozungumza kwa niaba ya wenzao Eva Kileo na Joseph Munishi kutoka kikundi cha Jitegemee Muungano wameishukuru Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuendelea kuwapatia fursa za mikopo hiyo huku wakiahidi kurejesha kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai imetoa jumla ya shilingi 213,400,000 kama mkopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kuanzia mwezi Julai 2021 ikiwa ni fedha za makusanyo ya ndani pamoja na marejesho ya mikopo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai