Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi Mil. 118 na laki 5 kwa vikundi 16 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wilayani humo.
Akikabidhi mkopo huo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka amesema kuwa fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani pamoja na marejesho ya vikundi vilivyopita na kusema kuwa vikundi vilivyopata mikopo vinapaswa kurejesha mkopo huo kwa wakati ili vikundi vilivyokosa awamu hii vipate kwani wahitaji ni wengi.
Rutaraka amesema kuwa idara ya maendeleo ya jamii inayosimamia vikundi hivi inapaswa kuwashirikisha madiwani wa kata husika ili kuweza kupata vikundi vyenye sifa ili kuepukana na usumbufu wa marejesho na fedha hiyo iweze kuzalisha kama ilivyokusudiwa kwa tija ya halmashauri na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Hai Deonis Myinga amesema kuwa mkopo huu ni utekelezaji wa sheria ya fedha za serikali za mitaa sura ya 290 yenye kanuni zilizotungwa chini ya kifungu 37(a) kifungu kidogo cha nne ambayo ni kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi na vya wanawake ,vijana na walemavu iliyotungwa mwaka 2019.
Myinga amesema kuwa wao kama halmashauri wanakusanya mapato ya ndani yanayotokana na makusanyo ya ushuru kutoka sehemu mbali mbali za biashara na kutenga asilimia kumi katika vikundi hivyo na wanakopesha kila baada ya miezi mitatu
Nae mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Hai Wanguba Maganda amesema kuwa ni vyema vikundi hivyo kutumia fedha hizo kwa lengo kusudiwa ili waweze kurejesha kwa wakati na warudishe kama kikundi na si kwa mtu mmoja mmoja kwani kuna baadhi ya vikundi wakipata mkopo wanagawana jambo ambalo sio sahihi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai