Halmashauri ya wilaya ya Hai imekabidhi kiasi cha shilingi milioni mbili kwa familia mbili za walimu kufuatia ajali ya moto uliozuka majira ya saa 8 usiku wa kuamkia Disemba 29, 2022 na kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja na vitu vyote vilivyokuwamo ndani ya nyumba hiyo katika kitongoji cha Nyerere kata ya Muungano wilayani humo.
Akikabidhi fedha hizo kwa waathirika wa ajali hiyo ya moto, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Hai Edmund Rutaraka ambaye pia ni diwani wa kata ya Muungano ametoa pole kwa familia hizo na kuwataka kuwa na subira ikiwa ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwa hakuna vifo wala majeruhi.
“Sisi kama halmashauri ya wilaya ya Hai tumeona tuje tuwashike mkono kwa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila familia ili muweze kuona ni kitu gani cha muhimu cha kuanza kufanyia kazi haraka wakati tunaendelea kuwatafuta wadau mbalimbali kuweza kusaidia familia hizi, poleni sana na tunaamini ni mipango ya MwenyeziMungu kwa sababu pameungua lakini hakuna kifo wala majeruhi yoyote”
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Dionis Myinga akizungumza katika eneo la tukio leo asubuhi amewapa pole kwa kupotelewa na mali zao zote kufuatia ajali hiyo ya moto na kueleza kuwa.
“baada ya kuwa wamepotelewa mali zao zote kwa ajali hii ya moto kimsingi bado wanahitaji mahitaji mbalimbali kama vile chakula, malazi na mavazi hivyo kama halmashauri tukaona ni busara tuangalie chochote kinachoweza kupatikana kwa ajili yao”
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo ,Rahel Shedafa kwaniaba ya familia hizo amewashukuru viongozi wa Halmashauri Kwa kuwambilia katika kipindi kigumu wanachopitia.
Walimu hao Zanika Solomon na Raheli Shedafa walikuwa wamepanga katika nyumba inayomilikiwa na wakala wa majengo Tanzania TBA ambapo nyumba hiyo pamoja vitu vyote vilivyokuwa ndani vimeteketea kwa moto ambao ulizuka usiku wa manane na chanzo chake bado hakijajulikana.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai