Katika utekeleza Sera ya Elimu bure, kata ya Masama kati wilayani Hai imepokea jumla ya shilingi million 63, 759,724 kutoka Serikalini katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa shule 6 za msingi na sekondari 2 zilizopo kata hiyo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM katika kata hiyo Diwani wa kata ya Masama kati Kandata Kimaro amesema kati ya fedha hizo, shilingi million 33, 823, 724 zimetolewa kwa ajili ya elimu msingi ambapo shilingi million 24, 636, 000 zilitolewa kwa ajili ya elimu sekondari.
“Fedha hizi zimeleta ahueni kubwa sana kwa wananchi, wanafunzi hawatakiwi kuchangia ada ya shule hivyo Serikali katika jitihada zake za kuongeza ufaulu shuleni pia imetupatia nyongeza ya waalimu 12”
“Vilevile katika kuboresha miundombinu ya shule kata yetu kupitia Serikali kuu, Halmashauri, mfuko wa jimbo, pamoja na jitihada za kata pamoja na wananchi na wahisani imeweza kunufaika ambapo kupitia ofisi ya mbunge tulipata saruji mifuko 50 na mabati 60 katika shule ya msingi Mafeto”
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai Wang’uba Maganda amewaomba viongozi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano kwa diwani huyo ili kuendelea kuitekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai