Utalii wa ndani umekua ukihimizwa na viongozi mbalimbali ikiwemo wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ikiwa njia nzuri ya kuongezea Taifa pato pamoja na kuthamini rasilimali za taifa.
Hayo yamebainika baada ya timu ya wataalam halmashauri ya wilaya ya Hai kutembelea eneo linaloitwa Sieni lilipo Masama katika ziara iliyolenga kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii kwa lengo la kuangalia namna ya kuviboresha na hatimaye kuanza kutumika.
Akizungumza katika ziara hiyo Afisa utalii wilaya ya Hai Amani Temu amesema vivutio hivyo vya utalii ni muhimu kwa wilaya ya Hai endapo vitaboreshwa kutokana na historia ya eneo hilo kuwa ni ya kipekee kwani kuna eneo ambalo linaitwa daraja la mungu ambalo ni daraja lililojijenga lenyewe kwa mawe pekee.
“pamoja na huu uzuri unaonekana hili daraja likiwekewa vizuizi ili mtu ajishike asione kizunguzungu litatuingizia sana kipato kwasababu watalii watatamani kuja hapa kuona hilo daraja la mungu lipoje na kwanini liitwe hivyo kuna historia gani hapa hiyo ni hatua tosha ya kuongeza pato la nchi kwa watalii wa ndani na wa nje wakija hapa kuona daraja hili, kwakweli tuthamini vya kwetu”.
Miongoni mwa wa watu waliokuwa kwenye ziara hiyo ni mchungaji Walter Kimaro aliyeishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na kuelezea kuwa eneo hilo ni sehemu ambayo watu walikuwa wanaenda kufanya ibada na kuomba baadhi ya vitu huku wakienda wakati mwingine wanavikuta.
Ameongeza kuwa eneo hilo lilikuwa na mapango ambayo watu walikua wanajificha wakati wa vita vya wenye kwa wenyewe(wamachame na wakibosho).
Pia eneo hilo lilikuwa likitumika kuangalia utabiri wa matukio ya mwaka kama vile njaa, ugonjwa, ukame pamoja na mvua lakini kwa zama za sasahivi hicho kitu hakipo tena.
“nilifahamu eneo hili mwaka wa 61 nikiwa mdogo sana kipindi hicho ukitaka kuongea na mababu lazima uingie huko kwenye mapango , walikuwa wanaenda na vitu vya kuchinjachinja na pombe saa nyingine , na sio kila mtu alikua anapaswa kuingia huko ilikua ni watu maalumu na mpaka ukristo ulipoingia waliacha mila hizo zilionekana hazina maana japo kweli ulikua ukiomba unapata kabisa”.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Hai David Lekei amesema anatambua eneo hilo kama eneo muhimu sana na maeneo kama hayo ni lulu kwa taifa na ni maeneo ya kipekee ya kuweza kutuingizia kipato.
“ tunashukuru sana kwa mapokezi tuliyopata nadhani hili eneo linapaswa liandikiwe historia ili watalii wakianza kuja wapate historia kamili hili eneo ni la kipekee kwakweli siajawahi kuona eneo kama hili nashukuru sana uongozi wa kijiji pamoja na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Hai kwa kuweza kushirikiana kufahamu sehemu kama hii hivyo tuhimizane tuanze wenyewe kuwa watalii na tuyatunze haya maeneo kwa vizazi vijavyo na kwa Taifa pia kwenye kuongezea pato nchi hili eneo liandikiwe historia kwakweli naomba sana”.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai