Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepokea kiasi cha shilingi 206,579,835 kutoka ubalozi wa Japan kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya msingi kibohehe.
Fedha hizo tayari zimepokelewa kwenye akaunti ya mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo tawi la NMB tawi la Hai na kwa sasa Halmashauri ipo kwenye taratibu za kupata mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Akizungumzia upatikanaji wa fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ndugu Yohana Sintoo amesema zimepatikana baada ya halmashauri kuwasilisha andiko kwenye ubalozi huo kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya shule hiyo ambayo iliangushwa na upepo mkali huku akiwashukuru wadau na wananchi waliojitolea kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.
“nipende kuushukuru ubalozi wa Japan kwa kutupatia fedha hizi ambazo zitenda kujenga madarasa na ofisi za waalimu,pia niwashukuru wanachi wa kibohehe ambao wamejitoa kwa kuchangia na kufanya kazi za mikono ambazo thamani yake ni kubwa” amesema Sintoo.
Zaidi ya wanafunzi 150 walilazimika kuhamishiwa kwenye shule za jirani baada ya majengo ya shule hiyo kuezuliwa na mengine kuangushwa na upepo mkali ambapo hadi sasa juhudi zinafanywa ili kuijenga shule hiyo upya.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai